26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ron Dennis astaafu Fomula One

Ron Dennis.SURREY, LONDON

MKURUGENZI wa timu ya magari ya Fomula One, Ron Dennis, ametangaza kustaafu baada ya kuutumikia mchezo huo kwa miaka 35.

Mkurugenzi huyo mwenye umri wa miaka 69, amesema huu ni wakati sahihi wa kustaafu mchezo na kuwapisha vijana waendelee kutoa michango yao na kuufikisha mbali.

Dennis alikuwa mkurugenzi katika timu ya magari ya McLaren. Kiongozi huyo alitoa taarifa ya kustaafu kabla ya kufanya mazungumzo na timu yake, lakini baada ya muda alitoa taarifa kwa uongozi wake na kisha taarifa hiyo kuenea kupitia mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, Dennis amedai kuwa anastaafu lakini bado ataendelea kutoa mchango wake kwa vijana kama ushauri kutokana na uzoefu alioupata kwa kipindi chote cha miaka 35.

Mkurugenzi huyo ameacha ujumbe ndani ya timu hiyo akielezea mafanikio waliyoyapata kwa kipindi chake na kuutaka uongozi uliopo kupambana kwa ajili ya kuifikisha timu hiyo mbali.

“Tangu nikiwa hapa, timu ilikuwa inafanya vizuri hasa katika biashara, ninaamini watu ambao wamebakia wataendelea kufanya hivyo kwa ajili ya kuongeza mafanikio zaidi.

“Nimefanya maamuzi sahihi lakini pia ni maamuzi magumu, ila kila kitu kina wakati wake na nadhani huu ulikuwa ni wakati wangu sahihi wa kustaafu na kuwapisha wengine waipeleke mbali zaidi.

“Kwa kipindi change, nilihakikisha McLaren inashinda mataji makubwa duniani ambapo tulifanikiwa kuyachukua 20, tukaweza kuingiza fedha pauni milioni 850 kwa mwaka katika biashara zetu.

“Biashara iliweza kwenda vizuri na nilifanikiwa katika uongozi wangu kuongeza ajira ambapo tuliweza kuwaajiri wafanyakazi 3,500, hivyo naweza kujivunia baadhi ya mambo ambayo yalifanyika kwa kipindi changu,” alisema Dennis.

Taji la kwanza chini ya uongozi wa Dennis lilipatikana 1984 kupitia kwa dereva wake, Niki Lauda, huku taji la mwisho la dunia lilipatikana 2008 kupitia kwa dereva wake, Lewis Hamilton.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles