33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi zungumzeni na watoto – Polepole

MKUU wa Wilaya ya Ubungo, Hamphrey  Polepole
MKUU wa Wilaya ya Ubungo, Hamphrey Polepole

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

MKUU wa Wilaya ya Ubungo, Hamphrey  Polepole, amewataka wazazi kutenga muda wa kuzungumza na watoto wao wajue mahitaji na changamoto wanazokumbana nazo shuleni.

Pia amewataka waweke kipaumbele kwa kuwa na bajeti maalumu ya elimu waweze kulipa ada kwa wakati jambo ambalo litasaidia walimu kuwa na ari ya kufundisha

Hayo yaliyasema   Dar es Salaam juzi katika hotuba  iliyosomwa kwa niaba yake na Ofisa Tarafa wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Mbarawa katika mahafali ya wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Precious iliyopo Goba.

Alisema   ni vema wazazi wa hasa wa kiume warudi nyumbani mapema   waweze kuzunguza na watoto wao.

Wazazi wengi wamebatizwa jina la  ‘wanyama wa usiku’ kwa kuwa wanarudi usiku kila siku jambo ambalo linawafanya washindwe kuzungumza na watoto wao, alisema.

Alisema jukumu la kulea watoto ni la jamii nzima wakiwamo wazazi na walimu.

Alishukuru uongozi wa shule hiyo  kwa kubeba jukumu la kutoa elimu kwa watoto wa Tanzania na kwamba Serikali inaunga mkono juhudi za sekta binafsi.

“Watoto wakipewa elimu itakuwa mkombozi katika maisha yao na wazazi ni lazima muweke  mkazo kuhakikisha mnawalea katika maadili mema katika kipindi chote cha maisha yao.

“Kwa sababu  tukiwa na watoto waliopata maadili mazuri kwa hakika taifa letu litaweza kusonga mbele kwa kuwa na raia wema na wenye hofu ya Mungu,” alisema.

Mkurugenzi wa shule hiyo, Damas Ngoiya, alisema elimu ndiyo nguzo muhimu ya kumlea mtoto na huo ni urithi mzuri na kudumu.

Aliiomba Serikali kupambana na watu wanaoanzisha shule holela huku baadhi yao wakigeuza nyumba zao kuwa shule.

Aliwapongeza wazazi na serikali kwa namna wanavyompa ushikiano katika kuhakikisha watoto wa Tanzania wanapata elimu bora.

Alisema shule yake ilianzishwa kwa kufuata utaratibu wa serikali na mwaka huu wanafunzi wamefikia darasa la tano huku akisisitiza kwamba lengo la kuanzishwa kwake ni kutoa elimu bora kwa gharama nafuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles