28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaotumia maji ya Ziwa Victoria watahadharishwa

01-mwanza-rock-city-tembea-tanzania

Na BENJAMIN MASESE,

WANANCHI wa mikoa inayozunguka Ziwa Victoria wameaswa kuacha kuchota au kutumia maji yenye  rangi ya kijani na maziwa.

Mtaalamu wa Usimamizi wa Misitu wa Mradi Hifadhi ya Mazingira katika Bonde la Ziwa Victoria (LVEMP II), Simon Msemwa amesema maji hayo   yamepoteza ubora wake kutokana na kuzidiwa na uchafu wa unaotokana na kinyesi na kemikali.

Alikuwa akizungumza na Kamati ya Mahesabu ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) ilipotembelea miradi  ya maendeleo inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB).

Msemwa alisema  vitu vinavyochangia maji ya Ziwa Victoria  kuchafuka ni     shughuli za binadamu zikiwamo uvuvi haramu, kilimo pembeni  mwa  ziwa na ujenzi wa makazi ya watu karibu na mito au  ziwa.

Sababu nyingine ni mafuta ya  vyombo vya usafiri wa majini, kemikali kutoka viwandani na utupaji ovyo wa takataka ngumu.

Msemwa alisema zipo sehemu  pembeni mwa Ziwa Victoria maji yake yamefikia hatua ya  kubadilika  na kuwa na rangi ya kijani au maziwa  kutokana na uchafu .

Alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wakiyatumia kwa matumizi mbalimbali jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.

“Naombeni kuwaomba wananchi kuacha  kutumia maji yenye rangi hizo kwa sababu  yanakuwa na uchafu uliozidi,  maana ipo migodi, viwanda na shughuli zingine za kilimo hususan bustani ambazo  mara nyingi hutumia  dawa.

“Katika vyombo vya usafiri vimekuwa miongoni mwa vitu vinavyochafua  maji, mfano meli za zamani hazina mfumo wa kuhifadhi taka.

“Kwa sababu hiyo  kinyesi huingia moja kwa moja majini …ndiyo imefikia hatua ya Sumatra kuja na sheria ya meli mpya kuwa na kontena la taka,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles