Na Judith Siaga, TUDARCo
Timu ya soka ya Manispaa ya Kinondoni, KMC imeanza kambi rasmi leo Agosti 26, kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara mkoani Morogoro.
Ofisa Habari KMC, Christina Mwagala amesema kambi hiyo itakuwa ya siku 21 ikihusisha michezo ya kirafiki.
Christina amesema kutakuwa na programu mbalimbali za mazoezi ili kufanya kikosi chao kiwe vizuri msimu wa 2021/2022.
Kuhusu usajili amesema KMC ilikuwa inafanya kimya kimya, kwa sasa wamefikia katika hatua za mwisho na siku yoyote watawatangaza wachezaji ambao wamewasajili.
Amewaomba mashabiki wa timu hiyo na kuwatoa hofu kuwa wamesajili wachezaji wazuri na wapinzani wajiandae.