23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

29 WAPANDISHWA VYEO MAGEREZA

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM


AMIRI Jeshi Mkuu, Rais Dk. John Magufuli, amewapandisha vyeo maofisa watano wa Magereza kuwa naibu kamishna.

Mbali na hao, pia Rais Magufuli amewapadisha maofisa wengine 24 kuwa makamishna wasaidizi waandamizi wa jeshi hilo kuanzia Mei 25, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, iliwataja waliopandishwa kuwa Naibu Kamishna wa Magereza, ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Uwesu Ngarama, Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza Dar es Salaam; Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Gideon Nkana, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Dar es Salaam na Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Jeremiah  Nkondo, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera.

Wengine ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Tusekile Mwaisabila, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi na Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Augustine S. Mboje ambaye ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam.

Waliopandishwa vyeo kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi ni Kamishna Msaidizi, Mbaraka Semwanza, Mwalimu wa Hisabati na Kemia Shule ya Sekondari Bwawani; Kamishna Msaidizi, George Mwambashi, Mkuu wa Kitengo cha Sheria Makao Makuu; Kamishna Msaidizi, Charles Novat, Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo Makao Makuu; Kamishna Msaidizi, Faustine Kasike, Mkufunzi Mwandamizi Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) Kunduchi, Dar es Salaam.

Mbali na hao, pia wapo Kamishna Msaidizi, Joel Bukuku, Mdhibiti wa Shirika la Magereza; Kamishna Msaidizi, Deogratius Lwanga, Ofisa Mnadhimu, Makao Makuu Ukonga; Kamishna Msaidizi, Boyd Mwambingu, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Pwani; Kamishna Msaidizi, Athuman Kitiku, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza; Kamishna Msaidizi, Hassan Mkwiche, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro; Kamishna Msaidizi, Luhende Makwaia, Mkufunzi Mkuu wa Mafunzo ya Kijeshi na Msaidizi wa Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira; Kamishna Msaidizi, Hamza Hamza, Ofisa Mnadhimu wa Mkoa wa Tabora; Kamishna Msaidizi, Jeremiah Katungu, Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Magereza Makao Makuu.

Wengine ni Kamishna Msaidizi, Mzee Nyamka, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro; Kamishna Msaidizi, Afwilile Mwakijungu, Mkuu wa Gereza Isupilo Mkoa wa Iringa; Kamishna Msaidizi, Ally Kaherewa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Ruvuma; Kamishna Msaidizi, Salum Hassan, Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Singida; Kamishna Msaidizi, Ismail  Mlawa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara; Kamishna Msaidizi, Chacha Jackson, Mdhibiti wa Fedha Makao Makuu na Kamishna Msaidizi, Rajab Bakari, Mkuu wa Kikosi Maalumu cha Kuzuia Ghasia  Ukonga, Dar es Salaam.

Mbali na hapo pia wapo Kamishna Msaidizi, Kijida Mwankingi, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mbeya; Kamishna Msaidizi, Julius Ntambala, Msimamizi Mkuu wa Ujenzi wa Nyumba 320 za Kuishi askari gereza la Ukonga; Kamishna Msaidizi, Mussa Kaswaka, Ofisa Mkaguzi Makao Makuu; Kamishna Msaidizi, Justine Kaziulaya, Mratibu Msaidizi Baraza la Usalama la Taifa na Kamishna Msaidizi, Bertha Minde ambaye ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Manyara.    

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles