2 CHAINZ, KESHA WARD WAFUNGA NDOA

0
1214

MIAMI, MAREKANI


RAPA Tauheed Epps, maarufu kwa jina la 2 Chainz, amefanikiwa kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Kesha Ward, huku mastaa mbalimbali wakijitokeza kwenye sherehe hiyo.

Rapa huyo alikuwa kwenye uhusiana na Kesha kwa muda mrefu, lakini miaka mitatu iliyopita waliamua kuweka wazi kila kitu na kuvishana pete ya uchumba.

“Ninashukuru sana, nimefanikiwa kufanya kile nilichokipanga kwa muda mrefu mjini Miami, kwa sasa nipo kwenye muunganiko na Kesha Ward, tumeweza kuwakutanisha marafiki karibu kwenye hoteli ya Villa Casa Casuarina,” aliandika 2 Chainz.

Baadhi ya mastaa ambao walionekana kwenye sherehe ya harusi hiyo ni pamoja na Kanye West na mke wake, Kim Kardashian, Alicia Keys na mume wake Swizz Beatz pamoja na Gucci Mane.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here