PRIYANKA, JONAS WAFUNGA NDOA YA KIMILA 

0
1010

MUMBAI, INDIA


HATIMAYE mwanamuzi na staa wa filamu nchini India, Priyanka Chopra, amefanikiwa kufunga ndoa ya kimila na mpenzi wake, Nick Jonas, walipokwenda kutambulishana mjini Mumbai, nchini India.

Wawili hao walitangaza kuwa wapo kwenye mipango ya kufunga ndoa, hivyo baada ya kuwasili nchini India wiki iliyopita kwa ajili ya kukutanisha familia zote, upande wa mwanamke Priyanka wakaomba wawili hao wafunge ndoa ya kimila kwanza na baada ya hapo wataendelea na utaratibu wao wa ndoa waliyoipanga.

Kupitia ukurasa wa Instagram, mrembo huyo alithibitisha kukamilisha hatua za awali za kimila ambazo ni kama ndoa kwa kuzikutanisha familia zote mbili.

“Moyo wangu kwa sasa upo kwa Jonas, kila kitu kimekwenda sawa na sasa ninaweza kuitwa Mrs Jonas, taratibu za kimila zimekamilika na mambo mengine yataendelea,” aliandika mrembo huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here