WAZIRI ATUMIA USAFIRI WA BAISKELI KWENDA KLINIKI

0
734

WELLINGTON, New Zeiland


WAZIRI anayeshughulikia masuala ya wanawake nchini hapa amelazimika kuendesha baiskeli  kwenda hospitali kwa  wiki 42 kwa ajili ya kujiandaa kujifungua mtoto wake wa kwanza kwa kile ambacho anadai hawakuwa na nafasi ya kutosha ndani ya gari lao na mumewe kwa ajili ya watoa huduma.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Waziri huyo kutoka chama cha  Green,  Julie Genter,  alisema   mbali na kukosekana nafasi  katika gari hilo, alilazimika kutumia usafiri huo  ikiwa ni sehemu ya mazoezi ya kijiweka vizuri katika nafya.

Kupitia    ujumbe na picha ambazo azilizutuma jana katika mtandao wake wa  jamii wa Instagram aliandika kwamba yeye na mumewe walikuwa wanaifurahia asubuhi hiyo njema.

“Kitu hiki ndicho kinachotupa bahati,” aliwaandikia wafuasi wake kupitia mtandao huo   wa  jamii.

“Mimi na mume wangu  tulipanda baiskeli kwa sababu hapakuwa na nafasi ya kutosha katika gari kwa ajili ya  wafanyakazi wa msaada … lakini pia iliniweka mimi katika hali nzuri zaidi.

“Safari ya kutumia baiskeli ya umeme ilikuwa ni nzuri  kwa kiasi kikubwa naifurahi  safari hii na tunatarajia kuongeza nafasi nyingine kwenye baiskeli yangu kwa ajili ya mtoto atakayekuja wiki chache zijazo,”aliongeza.

Endapo atajifungua waziri huyo ambaye atachukua   miezi mitatu kwa ajili ya mapumziko atakuwa ameongeza idadi ya wanasiasa ambao  wamejifungua wakiwa madarakani.

Mbunge wa kwanza nchini hapa kujifungua ilikuwa ni mwaka 1970 na mwingine mwaka 1983.

Mwaka  2016 Australia ilibadilisha sheria zake kwa kuwaruhusu viongozi wanawake kunyonyesha wakiwa ndani ya bunge.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here