25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatakiwa kulikagua baraza la wafugaji kufahamu matumizi ya shilingi bilioni 22

Na mwandishi wetu.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafugaji Tarafa ya Ngorongoro (NPC) wameiomba serikali kufanya ukaguzi maalum matumizi ya fedha ya baraza hilo ili kuondoa mgogoro wa chini kwa chini uliopo baina ya viongozi wa baraza hilo na wajumbe wake.

Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kufuatia tuhuma walizoeleza kuwa kumekuwa na ulaji mkubwa wa fedha za baraza kinyume cha taratibu za matumizi ya fedha.

Wajumbe hao hawakutaka majina yao kutajwa na gazeti hiki wameeleza kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita baraza lilipokea zaidi ya shilingi bilioni 22 kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi lakini hakuna uwazi wowote katika matumizi ya fedha hizo.

“Baraza hili limeanzishwa ili wajumbe wote tunufaike nalo pamoja na wananchi tunaowaongoza lakini wamekuwa wakifaidika watu wachache kwa safari za hapa ana pale huku wengi wetu tukikosa hata posho hasa pale tunapohudhuria vikao mbalimbali hali inayotufanya tuishi katika mazingira magumu katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku”,alisema mjumbe mmoja wa baraza hilo.

Wameongeza kuwa viongozi wao wanakiri kupokea fedha kutoka ndani na nje ya nchi zaidi ya shilingi bilioni 22 lakini hakuna anayejua mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo zaidi ya watu wachache inaoelezwa kuwa shilingi bilioni 12.5 zimetumika kwa safari za viongozi wa juu kutoka Karatu kwenda Arusha, Dar es salaam na Nairobi nchini Kenya.

Pia inadaiwa kuwa mmoja wa kiongozi wa juu wa baraza hilo ametumia takribani shilingi milioni 6 za baraza hilo kwa ajili ya kumlipia ada mtoto wake anayesoma nchini Uganda kitu ambacho ni kinyume na taratibu za baraza hilo.

Juhudi za kumpata Msajili wa Taasisi zisizo za kiserikali katika mkoa wa Arusha kuelezea kuhusiana na uendeshaji wa baraza hilo kwa sasa hazikuweza kuzaa matunda baada ya simu yake kutopatikana huku viongozi wa baraza hilo nao wakishindwa kupatikana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles