24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ndalichako aunda kamati kumfuatilia mkandarasi

MWANDISHI WETU-RUKWA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa  Joyce Ndalichako, amesema ameunda kamati itakayofuatilia shughuli za mkandarasi anayeendelea na ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (Veta) mkoani Rukwa alivyopata zabuni na kumtaka ajieleze.

Pamoja na hali hiyo, alisema mkandarasi huyo ameidanganya Serikali katika mkataba wake ulioonyesha uwepo wa vifaa vya kazi katika eneo la ujenzi huku eneo hilo likiwa tupu na kazi zake kufanyika bila ya wataalamu na vifaa vilivyoorodheshwa kwenye mkataba.

Alisema kamati hiyo pia itashughulikia kuona endapo thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali inaendana na majengo yaliyojengwa katika eneo hilo ambalo yalitakiwa kujengwa majengo 22, ambapo hadi sasa ni majengo 13 tu kikiwepo kibanda cha mlinzi ndio yameanza kuinuka.

Hayo yalisemwa mwishoni wa wiki mjini Sumbawanga, ambapo alimtaka mkandarasi huyo kuhakikisha anakabidhi majengo hayo Septemba mwaka huu, ambapo hadi sasa ujenzi huo umefikia asilimia 25 tofauti na makubaliano ya mkataba aliotakiwa kufikia asilimia 61 hadi Mei.

 “Wakandarasi wanaofanya kazi na Wizara ya Elimu badilikeni, kwa kweli miradi yangu yote nitaendelea kuipitia na nitaendelea kuchukua hatua kali kwa wale wakandarasi ambao wanapata kazi kiujanjaujanja, kwanza nitashughulika na watu wangu wa kitengo cha manunuzi, hebu angalia vifaa kama hivyo,” alisema Prof Ndalichako.

Alisema baada ya kutembelea ujenzi wa Veta katika eneo hilo la Kashai lililopo katika Manispaa ya Sumbawanga na kuonyesha kutoridhishwa na kuelekeza kuwa kabla ya kuendelea na ujenzi huo, lazima vifaa vinavyotumika katika ujenzi vipimwe kuonyesha kama vinastahili ama vinginevyo viondolewe katika eneo la ujenzi na mkandarasi huyo kuleta vifaa vingine kwa gharama yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles