22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Wabunge Uingereza kupiga kura ya tatu

LONDON, UINGEREZA

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Theresa May, anakabiliwa na uwezekano wa kushindwa kwa mara nyingine iwapo nchi  hiyo itashindwa katika jaribio lake la kujitoa katika Umoja  wa Ulaya, maarufu kama Brexit, bila makubaliano ifikapo Aprili 12, mwaka huu.

Wabunge wa nchi hiyo, jana walitarajiwa kupiga kura ya tatu bungeni katika mpango wa Brexit, ambapo May alielezea alipofikia na Umoja wa Ulaya, na kueleza sababu za Uingereza kushindwa kujiondoa rasmi kwenye umoja huo.

Kwa mujibu wa Gazeti la Times, kuna nafasi ndogo kwa May kupata wingi wa kura, huku chama cha upinzani cha Labor, chama cha Democratic Unionist cha Ireland Kaskazini na baadhi ya wajumbe wasiokuwa na imani na Ulaya kutoka kwa chama cha Conservative wakiapa kupinga mpango huo.

Serikali imesema kura iliyopigwa jana ni kuhusu makubaliano ya Uingereza kujiondoa, na si tamko tofauti la kisiasa kuhusu mahusiano ya siku za mbele kati ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya walikubali kuongeza muda ya Brexit hadi Mei 22, mradi tu makubaliano ya kujiondoa yaidhinishwe na Bunge la Uingereza wiki hii.

Kama hayataidhinishwa, walikubaliana kuongeza muda wa mchakato huo hadi Aprili 12 mwaka huu, ambapo Uingereza kabla ya hapo itahitajika kutoa mapendekezo ya namna ya kusonga mbele na suala hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,415FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles