22.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Bifu la Lyyn, Tanasha Kivuli cha usaliti kinavyomtesa Mondi

SWAGGAZ RIPOTA

BAADA ya kukaa nje ya skendo kwa muda mrefu, hatimaye staa wa muziki, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, amerudi kwa kasi akijiingiza kwenye vita ya maneno na mrembo Irene Louis maarufu mtandaoni kama Lyyn.


Hatua hiyo imekuja baada ya Diamond kulazimika kumjibu Lyyn ili kutetea penzi lake kwa Tanasha baada ya mrembo huyo kutumia muda mwingi kutangaza kuwa anatoka kimapenzi na Mondi.


LYYN NI NANI?
Huyu ni mrembo toka Buguruni, Dar es Salaam aliyeanza kujipatia umaarufu kupitia video za muziki wa Bongo Fleva kama video vixen. Mara ya kwanza, Lyyn alionekana katika video ya Kwetu ya msanii wa WCB, Rayvanny.


Baada ya kuonekana katika video hiyo, uzuri wake uliendelea kumpa umaarufu mtandaoni akajikuta kwenye skendo ya kuchepuka na Diamond Platnumz wakati akiwa na Zari The Boss Lady.


Lyyn, hakusika kutangaza hadharani kuwa mara kadhaa, Zari akiwa hayupo Dar es Salaam, amekuwa analala ‘ikulu’ ya Madale kwenye kitanda cha Diamond Platnumz mpaka akafanikiwa kunasa ujauzito ambao kwa bahati mbaya ulitoka.


Licha ya Mondi, kuachana na Zari The Boss Lady, Lyyn aliendelea kujiweka karibu na Diamond kiasi cha kujiita simba jike kama vile Mondi anavyojiita simba dume.


Hivi karibuni Lyyn, aliweka picha ikimwonyesha amelalia kitanda kinachofanana na kile cha Diamond Platnumz, jambo ambalo liliibua hisia kuwa mrembo huyo huwa analala kwa Mondi kipindi ambacho Tanasha anakuwa yupo kwao, Kenya.


DIAMOND AVUNJA UKIMYA
Kupitia mtandao wake wa Instagram (Insta Stories), wiki hii, Diamond aliamua kuvunja ukimya kwa kuanika chati alizokuwa anafanya na mrembo Lyyn kupitia WhatsApp. Katika chati hizo zilionyesha Lyyn alikuwa akimtumia picha za mahaba ili kumtongoza Diamond amsaliti Tanasha.


Pia Diamond akionyesha msimamo mkali wa kutokuwa na nia ya kumsaliti Tanasha, kwani amekua na ameacha ‘utoto’ wa kuchepuka kama alivyokuwa anafanya zamani kwa kuwa penzi la mrembo huyo toka Nairobi Kenya limemtuliza.


Mondi, alionyesha kuchukizwa na tabia ya Lyyn, kutumia nguvu nyingi kuwaaminisha mashabiki kuwa anatoka naye kiasi cha kununua kitanda kinachofanana na kile cha Diamond ili tu ionekane huwa wanalala chumba kimoja jambo ambalo halina ukweli.


LYYN, TANASHA HAPATOSHI
Baada ya Diamond kutoa siri ya Lyyn kulazimisha mapenzi, mrembo huyo alitumia ukurasa wake wa picha kukanusha chati hizo akidai kuwa zimetengenezwa kama njia ya Mondi kujisafisha.


Tanasha, amekuwa upande wa Diamond, anaamini Lyyn amekuwa akitaka kumnyang’anya penzi lake na hayupo tayari kuamini kama Mondi anachepuka ndiyo maana naye alielekeza matusi mengi kwa Lyyn.


KIVULI CHA USALITI
Miongoni mwa mambo ambayo yameshika kasi mtandaoni kutokana na sakata hili ni historia ya Diamond kwenye sekta ya mapenzi. Mara kadhaa amekuwa akichepuka kwenye uhusiano wake imara.


Mfano alipokuwa na Wema Sepetu alichepuka hata alipoingia kwenye uhusiano na mama watoto wake, Zari The Boss Lady akachepuka na Hamisa Mobetto mpaka akampa ujauzito jambo ambalo linaonyesha wazi kivuli cha usaliti kimeendelea kumwandama staa huyo wa Bongo Fleva.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles