25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Polisi Kigoma waua majambazi watatu


 Na Editha Karlo


JESHI la Polisi mkoani Kigoma limewauwa watu watatu wanaosadikika kuwa ni majambazi    na kukamata risasi 42.

Inaelezwa majambazi hao  walikuwa wamejipanga kufanya uporaji katika baadhi ya nyumba za wananchi wilayani Kibondo.

  Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Louis Bura, alisema juzi usiku   polisi walipokea taarifa kutoka kwa wananchi  kuwa kuna majambazi walikuwa wanataka kuvamia baadhi ya nyumba.

Alisema   walifika eneo la tukio na   kurushiana risasi ambako askari mmoja,     James Mwita (37) na mama mmoja, Sophia Dicksoni (60) walijeruhiwa na   wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Kibondo.

Alisema askari huyo alipatiwa matibabu ya awali na sasa   amepatiwa rufaa   kwenda  kwenye matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na majeraha ya mguuni.

DC aliwapongeza wananchi kwa kuendelea kuonyesha ushirikiano  kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa wanay ifanya kwa kuwa ni kazi ngumu.

“Ujambazi unaotokea ni ujambazi unaoshirikiana na wananchi waliopo hapa wikayani kwetu.

“Naomba kutoa rai kwa wote wanaojihusisha  na matukio haya kuacha mara moja kwa kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua wale wote wanaojihusisha na matukio hayo,” alisema DC.

Amewataka wananchi kuacha kuwaingilia katika utendaji kazi wao kwa kuwa wapo baadhi wanawakamata wakiwatuhumu kwa ujambazi lakini ndugu zao wanawatetea na kudai siyo majambanzi.

“Niwaambie tu wananchi hatutavumilia kuona majambazi wanaendelea kututesa Kibondo tumechoka.

“Kuanzia sasa niwaombe wananchi wale wanaoshirikiana na raia wa Burundi kuvamia watu muache maana jambazi hawezi kuja bila kupewa taarifa na watu ambao wanafahamu ni nani ana fedha, ” alisema Bura.

Aliwataka wananchi kuacha kutoka nje   wanaposikia milio ya risasi kwa ajili ya usalama wao kwa kuwa ni hatari   kufuata milio hiyo inaweza sababisha madhara makubwa.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kibondo, Sebasitiani Pima, alisema walipokea watu watatu wakiwa wamefariki dunia na majeruhi wawili ambao wanaendelea kupatiwa matibabu.

Alisema mmoja wa majeruhi amehamishiwa  katika Hospitali ya Taifa  Muhimbili kwa matibabu zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,695FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles