30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

JPM awataka wanasiasa waige mfano wa viongozi wa dini

Anna Potinus – Dar es salaam

Wanasiasa nchini wametakiwa kuiga mfano wa viongozi wa dini nchini kwa kuheshimiana ili kuifanya nchi iwe na amani na kuachana na migogoro ya mara kwa mara.

Hayo yameelezwa leo na rais John Magufuli wakati akijibu hoja za viongozi mbalimbali wa dini Ikulu jijini Dar es salaam walipokutana kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu nchi.

“Ninataka vyama vyetu viige mfano mzuri wa viongozi wa dini mnavyoheshimiana hakuna anayemzuia Mbowe kufanya Mkutano kwenye jimbo lake la Hai au Kubenea kwenye jimbo lake la ubungo,” amesema.

“Nchi nyingine uchaguzi ukiisha unakuwa umeshaisha kila mtu anaenda kwenye maeneo yake na ndio maana sisi hatujawazuia wabunge kufanya mikutano kwenye majimbo yao kinachozuiliwa ni mtu kutoka kwenye jimbo lake na kwenda kwenye jimbo lingine kumtukana mwingine,” amesema.

Aidha amezungumzia suala la mchezo wa kamari ambapo amesema kuwa inawafanya watu wanajiwekea mawazo ya kuamini watashinda na kuwajenga hali ya uvivu na kuwataka vijana kufanya kazi kwa bidii.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles