ZIWA RUKWA HATARINI KUKAUKA

0
37

 

Na GURIAN ADOLF SUMBAWANGA

WAKAZI wanaoishi kwenye Bonde la Ziwa Rukwa, wilayani Sumbawanga, mkoani Rukwa, wameshauriwa kuongeza kasi katika kuhifadhi mazingira ili kuliokoa ziwa hilo linalokabiliwa na hatari ya kukauka.

Ushauri huo umetolewa jana na ofisa ufuatiliaji na tathmini wa Taasisi ya Kaengesa Environment Conservation Society (KAESO), Grace Shio, wakati wa semina ya kuzijingea uwezo asasi za kiraia mikoa ya Rukwa na Katavi kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Alisema kuwa, wakazi waishio katika Bonde la Ziwa Rukwa wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanatunza mazingira, ikiwa ni pamoja na kuacha tabia ya kukata miti hovyo, kupunguza mifugo na kulima kandokando mwa ziwa hilo, kwani kumechangia kupungua kwa kina na ujazo wa maji yake.

Shio alisema kuwa, iwapo mambo hayo yataachwa bila kushughulikiwa katika kipindi cha miaka 30 ijayo, ziwa hilo litakauka na kupotea kabisa kwenye uso wa dunia.

Ofisa huyo alitoa wito kwa asasi mbalimbali kulivalia njuga suala la mazingira, hususan Bonde la Ziwa Rukwa, kutokana na umuhimu wake.

Alisema ziwa hilo linategemewa kwa shughuli za uvuvi, utalii na uwindaji, kwakuwa linapakana na Hifadhi ya Taifa ya Wanyamapori ya Katavi, huku ikiwa ni miongoni mwa maziwa machache yenye mamba wengi duniani.

 

Akichangia mada hiyo, mmoja wa wanasemina hao, Mussa Mwangoka, alisema changamoto kubwa iliyopo ni ukosefu wa elimu sahihi ya uhifadhi wa mazingira kwa wakazi waishio mwambao wa bonde la ziwa hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here