29.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 6, 2024

Contact us: [email protected]

ALI KIBA ASUBIRIWA FIESTA DODOMA

Na MWANDISHI WETU

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba, anayetamba na wimbo wake wa Seduce Me, anatarajiwa kutikisa wakazi wa Dodoma katika tamasha la burudani la Tigo Fiesta, litakalofanyika Ijumaa katika Uwanja wa Jamhuri.

Kiba tangu ameanza kupanda jukwaani katika Tigo Fiesta katika mikoa ya Arusha, Mbeya na Musoma, amekuwa akiwapagawisha mashabiki wa mikoa hiyo, kutokana na kuvutiwa na wimbo huo.

Wakazi wa Dodoma wameonyesha kufurahia uwepo wa Kiba pamoja na wasanii wengine watakaotoa burudani katika tamasha hilo.

Mmoja wa wakazi wa Dodoma, Juma Kibwana, alisema hatakosa katika tamasha hilo, kwani anampenda sana Ali Kiba kutokana na nyimbo zake kufanya vizuri, ikiwamo Seduce Me.

“Mimi kwa kweli sitakosa kwenye Tigo Fiesta kwa sababu najua shughuli ya Kiba, yaani jamaa ni mkali kinoma, nitakata tiketi yangu mapema ili nisipate usumbufu utakaosababisha nikose burudani,” alisema.

Wasanii wengine watakaopanda jukwaani katika Tigo Fiesta ni pamoja na Rostam, Ben Pol, Ali Kiba, Jux, Maua Sama, Nandy, Vanessa, Weusi, Barnaba, Darassa, Rich Mavocal, Beka, Mimi Mars, Country Boy, Moni Central Zone, Nedy Music, Zaiid, Genevieve, Nchama na Bright.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles