26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

AKON KUONGOZA TUZO ZA AFRIMA 2017

LAGOS, NIGERIA

NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Aliaume Badara ‘Akon’, anatarajiwa kuwa mshereheshaji katika utoaji wa tuzo za All Africa Music Awards (AFRIMA).

Tuzo hizo za awamu ya nne, zinatarajiwa kutolewa Novemba 12, wiki ijayo, kwenye ukumbi wa Eko Convention Centre, katika Hoteli ya Eko, jijini Lagos.

Kwa mujibu wa Tume ya Umoja wa Afrika na Kamati ya Kimataifa ya AFRIMA, imethibitisha kuwa, msanii huyo ambaye alizaliwa nchini Senegal, ataendesha shughuli yote akishirikiana na Sophy Aiida, raia wa nchini Cameroon ambaye ni mtangazaji wa runinga.

Akon alitumia ukurasa wake wa Instagram kuonesha furaha yake baada ya kupewa nafasi hiyo. “Nadhani nimepewa heshima kubwa sana ya kuja kuwa mshereheshaji wa AFRIMA, siyo kitu cha kukosa kwa wapenzi na wadau wa muziki,” alisema Akon.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles