25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 1, 2024

Contact us: [email protected]

WIZKID: NIMEWAHI KULALA NA WANAWAKE WAWILI

LAGOS, NIGERIA

NYOTA anayefanya vizuri katika muziki nchini Nigeria na Afrika, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’, amedai ustaa umemfanya alale na wanawake wawili kwenye kitanda kimoja.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 27, amedai aliweza kufanya hivyo baada ya kufanya kazi na wasanii wakubwa duniani, kama vile Chris Brown na Drake, hivyo wasichana wengi walikuwa wanajitokeza kwa jina lake kuwa kubwa.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, msanii huyo aliandika kwa lugha ya kikabila ijulikanayo kwa jina la Yoruba na kusema kwamba, kutokana na umaarufu wake, ameweza kulala na wasichana wawili kwa wakati mmoja.

“Nina furaha kubwa kwa maisha ninayoishi sasa, ubora wangu wa muziki na kufanya kazi na wasanii wakubwa kumenifanya nitembee na kila aina ya warembo, baada ya kufanya kazi na Chris Brown na Drake, warembo walikuwa wanajitokeza kwa wingi nikaweza kulala na wanawake wawili kwenye kitanda kimoja kwa kuwa wote walidai wananipenda,” aliandika Wizkid.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles