24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

ZITTO: NINA ORODHA YA WATU 348 WALIOPOTEA


Gabriel Mushi, Dodoma   |

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo), amesema anayo orodha ya watu 348 ambao wameripotiwa kupotea katika wilaya za kusini ambapo amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba kueleza kinachoendelea katika wilaya hizo.

Zitto ametoa kauli hiyo leo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambapo amesema kati ya watu hao 348, watu 68 wamethibitika kuwa kufariki dunia.

Amesema licha ya wizara hiyo kuomba bajeti ya Sh bilioni 945, kati yake Sh bilioni 596 sawa na asilimia 63 ya bajeti hiyo inaenda kwenye jeshi la polisi ambalo limeshindwa kuchunguza tukio la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

“Nina orodha ya watu 348 ya watu wa wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji, hatujajulimsha  watu wanaotoka Kilwa, kuna mtu jana amezungumza kuna orodha ya watu 1000 wamepotea, inawezekana orodha niliyonayo ambayo nitampatia waziri, watu 348 kati yao watu 68 wamedhibitika wamefariki. Tunaomba serikali itueleze nini kinaendelea wilaya za kusini ya Tanzania,” amesema.

Amesema mlolongo wa matukio ya watu wengi kutekwa na watu wasiojulikana na jeshi la polisi kushindwa kutoa maelezo yanaweza kutuletea shida kubwa ndani ya nchi.

“Mbunge Kilwa ndugu Bungara wa Kilwa amezungumza kwa hisia na wakati mwingine mwache watu wazungumze kwa hisiasa kwani wakati ndio wanaongea yale ambayo yanawahusu.

“Juni 12 mwaka jana, mama mmoja anaitwa Ziada Salum wa kitongoji cha maparani Kibiti, alichukuliwa na jeshi la polisi saa sita mchana, na leo ni miezi 11 mama huyo hajaonekana, kuna mtu anaitwa Rukia Mhoni na Tatu Mhoni  ni ndugu hawa, walichukuliwa na jeshi la polisi mpaka leo tunapozungumza miezi 11 hawajaonekana,” amesema Zitto.

Pamoja na mambo mengine, Zitto amesema kuna watu wana miaka miwili hawajulikani walipo akiwamo mwandishi wa habari Azory Gwanda na Ben Saanane, ambapo ameitaka serikali kutekelezwa matakwa ya katiba ambayo katika ibara ya 15 (1,2) inaweka wazi kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru.


 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles