22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

MBUNGE ATAKA WAPINZANI KUACHA KUTAFUTA ‘KIKI’

Gabriel Mushi, Dodoma

Mbunge wa Viti Maalumu, Ritha Kabati (CCM), amewataka wabunge wa vyama vya upinzani kuacha unafiki na kutafuta ‘kiki’ kwa kumkosoa Rais John Magufuli ndani ya Bunge lakini nje ya Bunge wanamsifia.

Pia amempongeza Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa kwa kutambua kazi nzuri ambazo zinafanyiwa na serikali ya awamu ya tano na kutambua Rais Magufuli anafanya kazi bila ubaguzi.

Kabati ametoa kauli hiyo leo wakati akichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi ambapo pamoja na mambo mengine alisema Msigwa sasa ameanza kukomaa kisiasa.

“Nimpongeze Rais alikuwa Iringa siku tano, amefanya kazi nzuri sana na wananchi wa Iringa wametambua uwepo wake, kwa mara ya kwanza nimpongeze Mchungaji Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini, kwa kutambua kazi nzuri ambazo zinafanyika katika awamu ya tano na kutambua Rais Magufuli anafanya kazi bila ubaguzi.

“Na maneno hayo mazuri ameongea mbele ya Waziri Mhagama (Jenister) wabunge na wananchi wa Iringa, kwa kweli nasema Msigwa sasa ameanza kukomaa kisiasa.

“Nashangaa wabunge wengine wa upinzani wanapokutana na Rais hawasemi haya maneno, hawamwambii ukweli,  lakini wanapoingia humu ndani kwenye Bunge, wanaanza kusema maneno mengine ni unafiki, hata jana wanasema Rais wetu hakosolewi, mbona mkikutana sasa hamumkosoi?

“Mnasubiri muongee humu bungeni muanze kukosoa muanze kutukana, mnataka kiki au mnataka nini,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles