24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri wa Afya aipa maelekezo MSD

AMINA OMARI-TANGA

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ameiagiza Bohari ya Dawa (Msd), kuhakikisha hadi kufikia leo Januari 15, mwaka huu wawe wamesambaza vifaa tiba katika vituo vyote vya afya nchini ambavyo vimefanyiwa maboresho. 

Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo, iliyoko mkoani Tanga.

Alisema kwamba, hadi sasa majengo mengi yamekamilika lakini Msd hawajapeleka vifaa tiba ili vituo hivyo viweze kuanza kutoa huduma za afya, jambo ambalo alisema hawezi kulivumilia. 

Alisema vituo hivyo ambavyo vipo ngazi ya halmashauri, vimeboreshwa ili kuweza kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali za wilaya na rufaa na kwamba, kitendo cha vituo hivyo kutofanya kazi, kinawafanya wananchi waendelee kupata shida katika suala la matibabu. 

“Nawaelekeza Msd kuhakikisha wanapeleka vifaa ili vituo hivyo viweze kuanza kutoa huduma mapema, kwani Serikali imetumia fedha nyingi kufanya maboresho ili kumsogezea huduma mwananchi wa hali ya chini.

“Kwa upande wa hospitali za rufaa, wizara imejipanga kusogeza huduma za madaktari bingwa katika hospitali hizo ili wananchi wasiweze kwenda umbali mrefu kufuata huduma za afya. 

“Yaani, hospitali zote za rufaa nchini zitakuwa na huduma ya magonjwa ya dharura, huduma za mama na mtoto pamoja na uangalizi maalumu kwa maana ya ICU, ” alibainisha Waziri Mwalimu.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Bombo, Dk. Asha Mahita, alisema uboreshaji wa huduma za afya mkoani humo, umeweza kusaidia wananchi wengi kukimbilia hospitalini kwa ajili ya kupata huduma za afya. 

Alisema kwa upande wa huduma ya mama na mtoto, idadi ya wajawazito waliofika katika vituo vya afya kupata huduma imeongezeka kutoka asilimia 60 hadi asilimia 90.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles