25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Mtoto wa tembo atumbukia shimoni Lwafi, aokolewa

Eliya Mbonea

Askari wa Pori la Akiba Lwafi, wamefanikiwa kuokoa maisha ya tembo mtoto aliyetumbukia ndani ya shimo kubwa jirani na Kijiji cha China mkoani Katavi.

Akisimulia tukio hilo lililotokea juzi, Mkuu wa Kanda Asubuhi Masunga amesema askari hao walifanikiwa kumuokoa tembo huyo kwa kuchimba njia ya kutokea kwenye shimo hilo kwa kujaza udongo.

“Jana jioni kundi kubwa la tembo wakiwa na watoto wakila ndani ya Pori la Akiba mpakani jirani na kijiji cha China, mtoto mmoja wa tembo alitumbukia shimoni.

“Baada ya kuona mtoto ametumbukia tembo wengine walijitahidi kumuokoa wakashindwa, wanakijiji hawakuweza kumuokoa kutokana na wingi wa tembo waliozunguka eneo hilo ila walichukua jukumu la kutaarifu uongozi waliofika na kutumia mbinu za uokozi usiku mzima na kufanikiwa kuokoa uhai wake,” amesema Masunga.

Amesema baada ya kuokolewa walikaa eneo hilo na mtoto wa tembo wakisubiri kundi la tembo lingeweza kurudi eneo hilo lakini halikurudi.

“Tumewasiliana na wadau wa Makoa Machame wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro wanaojishughulisha na kulea wanyama waliopoteza mama zao ambao walimchukua mtoto huyo na kumpeleka kwenye shamba lao kwa uangalizi wa karibu, wanasema tembo huyo anaendelea vizuri,” amesema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles