23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

WATEJA WAPYA NMB WACHANGIA MZUNGUKO WA BIL 10/-

Na JANETH MUSHI- ARUSHA


nmb

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, amesema wanajivunia  kuwa na wateja wanaochipukia ambao huchangia mzunguko wa fedha hadi kufikia Sh bilioni 10 kwa mwaka.

Pamoja na hali hiyo, alisema bado wanajivunia kuwa na mtandao mpana nchini ikiwamo kuwapatia mkopo unaofikia Sh bilioni 1.5, huku akiwakaribisha wateja na wasio wateja wa NMB kwa ajili ya kuwaonyesha fursa na bidhaa zake.

Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza katika mkutano wa uongozi wa benki hiyo pamoja na wateja wao mkoani hapa, ambapo alisema mpango huo ulianza mwaka 2014, ukilenga miji mikubwa sita  ambayo ni Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Morogoro, Arusha na Kilimanjaro na umeendelea katika miji mingine.

“Mpaka sasa, mtandao huu upo kwenye mikoa mitano tu ya Dar es Salaam, Mwanza, Morogoro, Mbeya na hapa Arusha.Tuna washirika zaidi ya 500 wa mtandao wa NMB Executive Network.

“Makusudi makubwa ya kuanzisha mtandao huu ni kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya benki na wateja wake na kuweka mahusiano yenye tija kwa pande zote mbili yaani kwa mteja na benki, huku tukiangazia wateja wakubwa tu,” alisema Ineke.

Akizungumzia faida kwa wateja, alisema suala la uwezeshaji kimaarifa huenda sambamba na utoaji wa elimu juu ya mipangilio ya biashara, elimu ya kodi pamoja na taratibu mbalimbali za Serikali juu ya biashara.

“Fursa ya kukutana na uongozi wa juu wa benki pamoja na menejimenti na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi. Na pia wafanyabiashara mbalimbali na kubadilishana mawazo.

“Lakini pia huwa tunatoa fursa ya kutoa mapendekezo juu ya bidhaa za NMB, mrejesho wa huduma za kibenki za NMB pamoja na kupata upendeleo kwa kupewa kadi maalumu za uanachama zinazokupa upendeleo wa huduma unapotembelea matawi yetu nchi nzima,” alisema Ineke.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles