24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wapigakura 504,133 kuamua Rais wa Z’bar

zecNa Mwandishi Wetu, Zanzibar

WAZANZIBAR 504,133, wanatarajia kutoa uamuzi kwa kupiga kura ya kuamua nani awe rais wa Zanzibar kati ya wagombea 14 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA ofisini kwake Maisara jana, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Salum Kassim Ali, alisema idadi hiyo imepatikana baada ya kukamilika kazi ya uandikishaji wapigakura wapya pamoja na uhakiki wa kuwaondoa watu waliofariki dunia.

Alisema kazi ya kuhakiki daftari la kudumu la wapigakura imekamilika, na hatua inayoendelea hivi sasa ni ya kampeni pamoja na kutoa elimu ya uraia kwa wananchi.

“Tuna wapigakura 504,133 watakaoshiriki  uchaguzi wa mwaka huu, baada ya kukamilika kazi ya kuhakiki daftari la kudumu la wapigakura,” alisema Ali.

Alisema majina ya watu 5,995 yamefutwa baada ya kuthibitishwa wamefariki dunia.

Ali alisema ZEC imejipanga vizuri kufanikisha shughuli za uchaguzi.

Aliwataja wagombea walioteuliwa na tume na tayari wameanza kampeni kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu, kuwa ni Rais Dk. Ali Mohamed Shein (CCM), Kassim Bakari Ali (Jahazi Asilia), Hafidh Hassan Suleiman (TLP), Said Soud Said (AFP), Maalim Seif Sharif Hamad (CUF) na Tabu Mussa Juma (Demokrasia Makini).

Wengine ni Mohammed Masoud Rashid (CHAUMA), Issa Mohammed Longa (SAU), Juma Ali Khatib (TADEA), Ali Khatib Ali (CCK), Khamis Iddi Lila (ACT-Wazalendo), Abdalla Kombo Khamis (DP), Hamad Rashid Mohammed (ADC) na Seif Ali Iddi (NRA).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles