28.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘WAPENI WATOTO BIMA YA AFYA BADALA YA NGUO’

Editha Karlo, Karagwe

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka amewataka wazazi na walezi mkoani Kagera kuhakikisha wanawapatia watoto wao zawadi ya kuwaingiza kwenye mpango wa Toto Afya kadi inayotolewa na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), ili wawe na uhakika wa matibabu pale wanapougua.

Mheruka ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji wa Kadi za Toto Afya na upimaji wa afya bure wa magonjwa yasiyoambukiza kwa wananchi.

“Mzazi au mlezi kumpatia mtoto zawadi ya kadi ya Toto Afya ni muhimu badala ya kumpatia zawadi ya nguo ambazo atazivaa na zitaisha.

“Ndugu zangu wazazi wenzangu baada ya kumaliza kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani zawadi nzuri ya kuwapatia watoto wetu ni kuwaingiza katika mpango huu kwani utamuwezesha mtoto kuwa na uhakika wa matibabu anapougua kwa kipindi cha mwaka mmoja,” amesema.

Kwa upande wake Meneja wa NHIF, Elias Odhiambo amesema wiki hii NHIF wanafanya zoezi la upimaji wa afya wananchi bure na kutoa Toto Afya kadi katika maeneo ya Omurushaka na Kayanga wilayani Karagwe.

“Nawaomba wananchi wote wafike maeneo ambayo tumeweka vituo kwa ajili ya kutoa huduma ili wapate huduma kwani huduma hizi ni bure,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles