24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

MAHIGA: WATANZANIA WAISHIO NJE HUTUMA FEDHA NYINGI

Maregesi Paul, Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga amesema Watanzania waishio nje ya nchi wanatuma zaidi ya Sh trilioni moja nchini kwa mwaka.

Waziri Mahiga ametoa taarifa hiyo bungeni jijini Dodoma leo Mei 23, wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/19.

“Watanzania hao wamekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa taifa kwa kuwa baadhi yao wamenunua nyumba zenye thamani ya Sh bilioni 29.7 kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

“Aidha, katika sekta ya afya, timu ya madaktari wa Kitanzania waishio Marekani kupitia taasisi ya afya, elimu na maendeleo ilitoa huduma ya afya bila malipo na vifaa tiba,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Mahiga amesema Tanzania kama nchi huru haiwezi kuchaguliwa maadui na marafiki duniani na kwamba itaendelea kushirikiana na mataifa mbalimbali duniani kulingana na jinsi itakavyoona inafaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,853FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles