30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

‘KULENI CHAKULA CHEPESI BAADA YA KUFUNGUA’

NA VERONICA ROMWALD-DAR ES SALAAM       |    


WAUMINI wa dini ya kiislamu waliopo katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, wameshauriwa kula chakula chepesi baada ya kufungua (futuru), kwani humsaidia mfungaji kutopata saratani ya utumbo.

Ushauri huo ulitolewa jijini Dar es Salaam jana na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) , Crispin Kahesa, alipokuwa akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalum.

“Kufunga ni ibada na ni jambo zuri kwa afya ya binadamu, lakini tunashauri watu kuzingatia kula vyakula vyepesi wakati wa kufungulia na si vile vigumu, kwa sababu vile vigumu huweza kuwasababishia matatizo ikiwamo saratani ya utumbo,” alisema.

Alisema wapo ambao hufungulia kwa kunywa maji au vyakula vya moto ni sahihi na bora zaidi kuliko wale wanaokula vyakula vigumu.

“Vyakula vyepesi ni kama vile uji, hivyo ndivyo ambavyo tunashauri na ukiwa wa moto kidogo ni mzuri kwa sababu unalifanyia tumbo lako ‘warm-up’, kulishtua kwani linakuwa limekaa muda mrefu pasipo kupata chakula,” alisema.

Alisema chakula cha daku nacho ni muhimu kwani humsaidia muhusika tumbo lake kutobakia tupu hadi jioni wakati wa ‘kufuturu’.

Pamoja na hilo, alisema mtu ambaye amewahi kuugua vidonda vya tumbo anakuwa kwenye hatari ya kupata saratani hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles