24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wachezaji EPL kukatwa bilioni 252 kusaidia klabu ndogo

London, England

WACHEZAJI wa Ligi Kuu England wanaweza kukabiliwa na kukatwa malipo ya zaidi ya Euro  milioni 100 (Sawa na zaidi ya Shilingi bilioni 252 za Tanzania)  kuzisaidia klabu za ngazi ya chini kujimudu kifedha kutokana na athari za mlipuko wa ugonjwa Corona.

Kama ilivyoripotiwa na The Sun, mazungumzo ya dharura yamefanyika kati ya Chama cha wachezaji wa kulipwa (PFA), Ligi Kuu na EFL juu ya jinsi ya kushughulikia athari za kifedha za zinazobabishwa na ugonjwa huo.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa, ingawa makubaliano bado hayajafikiwa na klabu za Ligi Kuu, kuna matumaini kwamba wachezaji watachukua hatua kusaidia klabu zilizo katika madaraja ya chini.

Ikiwa michezo haitachezwa hadi Julai, basi wachezaji klabu za Ligi Kuu wanaweza kukubali kupunguza  asilimia 20  ya mishahara yao kwa miezi mitatu ijayo ili kuzisaidia timu hizo.

Kwa hatua hiyo, wachezaji wa Ligi Kuu watakuwa wanatoa jumla ya Euro milioni 105 na inaaminika kuwa mshahara wa Machi hautakuwa tishio.

Serikali ya Uingereza imesimamisha ligi zote hadi angalau Aprili 30 kutokana na hofu ya kuenea kwa kasi kwa ugonjwa wa Corona uliozikumba baadhi ya nchi duniani.

Ligi Kuu, EFL na PFA zilikutana Ijumaa kujadili athari za kifedha za kusimamishwa kwa msimu.

“Ligi Kuu, EFL na PFA zilikutana leo na kujadili uzito unalioletw na janga la  Virusi vya COVID-19,” ilisema taarifa ya pamoja.

“Ilisisitizwa kuwa mawazo ya mashirika yote matatu yanaendelea kuwa na kila mtu aliyeathiriwa na virusi hivyo.

“Ligi Kuu, EFL na PFA zilikubaliana kwamba maamuzi magumu itabidi yachukuliwe ili kupunguza athari za kiuchumi za kusimamishwa  kwa shughuli za soka na kikazi nchini England na walikubaliana kufanya kazi kwa pamoja ili kufika suluhisho la pamoja,” ilisema taarifa hiyo.

Bodi hiyo itafanya mazungumzo zaidi wiki ijayo kuunda mpango wa pamoja.

Ronaldo kukatwa  bilioni 9 kulipa wafanyakazi Juventus

TURIN, ITALIA

MSHAMBULIAJI wa Juventus, Cristiano Ronaldo atapunguza mshahara wake kwa Euro milioni 3.8 (sawa na Shilingi bilioni 9.5 za Tanzania)  kwa mwaka ili kuisaidia Juventus kulipa mishahara wafanyakazi wengine ndani ya klabu hiyo katika kipindi hiki kigumu cha ugonjwa wa Corona.

Hatua hiyo imeokana na beki wa timu hiyo, Giorgio Chiellini kuzungumza na wachezaji wenzake kukubali kukatwa sehemu ya mishahara yao, akiwemo Ronaldo ambaye alipunguza kufikia Euro milioni 3.8 (sawa na Shilingi bilioni 9,597,160,000) za Tanzania.

Wachezaji na wafanya kazi wengine wa Juventus wamemaliza kipindi cha kujitenga kilichotokana na wachezaji watatu wa timu hiyo, Daniele Rugani, Blaise Matuidi na Paulo Dybala kuambukizwa virusi vya Corona.

Mtandao wa Tuttosport unaripoti kuwa nahodha wa Juve, Chiellini, ambaye bado amesalia katika hoteli ya  J Hotel,alizungumza kwa njia ya video na viongozi wa juu wa klabu baada ya kumaliza kuongea na Rais wa klabu hiyo,   Andrea Agnelli na Mkurugenzi, Fabio Paratici.

Alizungumza pia na wachezaji waandamizi wa timu hiyo , Gigi Buffon, Leonardo Bonucci na Cristiano Ronaldo, Chiellini alipata ushirikiano mzuri na kwa wachezaji wengine na aliwauliza kuhusu kukubali kukatwa mishahara wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa wa Corona unaoitesa Italia.

Makato hayo yanatarajiwa kupendekezwa  kulingana na mchezaji kwa kuhofia wachezaji wengine kupoteza mishahara yao, akiwamo Ronaldo ambaye atakatwa Euro milioni 3.8.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles