Corona yamfungisha ndoa ya kimya kimya mshambuliaji Azam

0
979

Jessca Nangawe -Dar Es Salaam

STRAIKA wa Azam FC, Shaban Iddi Chilunda,amefunga ndoa ya kimya kimya na mpenzi wake wa muda mrefu anayefahamika kwa jina la Bi Shammy.

Chilunda amefunga ndoa hiyo pasipo kualika watu, ikieleza sababu ya kufanya hivyo inatokana na kuwapo kwa tishio la ugonjwa wa corona, ambao umeuwa maelfu ya watu duniani.

Lakini pia ifahamke kuwa, Serikali imepiga marufuku shughuli zinazosababisha mikusanyiko ya watu, ikiwa ni tahadhari ya kuepuka kusambaa kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa huo vinavyofahamika kwa jina la Covid-19.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Chilunda alithibitisha kufunga ndoa hiyo na kusema anashukuru imefanikiwa.

“Namshukuru Mungu imemalizika salama, japo haikua na watu na nimefanya hivyo kutimiza masharti ya Serikali inayokataza mikusanyiko ya watu kutokana na janga linalotukabili kwa sasa,” alisema Chilunda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here