USHINDI WAMPA HISIA KALI ANCELOTTI

0
772

 

 

 

NAPLES, ITALIA


BAADA ya klabu ya Napoli kushinda mabao 3-2 dhidi ya AC Milan, kocha wa timu hiyo, Carlo Ancelotti, amefunguka na kusema kuifunga klabu hiyo kumemfanya akumbuke mbali sana

Katika mchezo huo Napoli ilianza kwa kuwa nyuma kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 49 kipindi cha pili yakiwekwa wavuni na Davide Calabria na Giacomo Bonaventura, lakini Napoli waliweza kusawazisha kupitia kwa nyota wake, Piotr Zielinski, aliyefunga mabao mawili na lingine likifungwa na Dries Mertens.
Ushindi huo umemfanya Ancelotti ambaye alikuwa kocha wa timu hiyo tangu 2001 hadi 2009, kuwa na hisia kali na kukumbuka wakati anaifundisha.

“Ni ushindi umbao umenifanya niikumbuke AC Milan wakati ninaifundisha, niliikumbuka klabu hiyo pamoja na wachezaji wake kama vile Gattuso ambaye kwa sasa ni kocha wao.
“Bado AC Milan ni timu bora nchini Italia, lakini katika mchezo huo hawakuwa tishio sana japokuwa waliweza kupata mabao mawili ambayo yalikuwa yanafanana,” alisema Ancelotti.

Kocha huyo alisaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo tangu Mei 23 mwaka huu kuchukua nafasi ya Maurizio Sarri. Mchezo wake wa kwanza kwenye ligi aliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lazio, Agosti 19.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here