MCHEZAJI WA BRAZIL AJIUNGA AL-SHABAB

0
5000
RIYADH, SAUDIA

ALIYEKUWA kiungo mshambuliaji wa klabu ya Toulouse inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ufaransa, Wergiton do Calmon, maarufu kwa jina la Somalia, amejiunga na klabu ya Al-Shabab ya nchini Saudia.
Al-Shabab FC ni klabu ya soka nchini Saudi Arabia ambayo ipo katika mji wa Riyadh. Timu hiyo ilianzishwa tangu mwaka 1947, huku ikiitwa jina la Shabab Al Riyadh, lakini mwishoni mwa mwaka 1967 walibadilisha jina na kujiita Al Shabab, ikiwa na maana ya Vijana.
Somalia ameichezea klabu ya Toulouse nchini Ufaransa kwa takribani miaka mitatu, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 raia wa nchini Brazil sasa amehamia katika klabu hiyo ya Al-Shabab.
Baada ya taarifa za mchezaji huyo kujiunga na klabu hiyo ya Al Shabab, idadi kubwa ya mashabiki kwenye mitandao ya kijamii walipigwa na butwaa wakidhani kuwa amejiunga na Al Shabab ambalo ni kundi la kijihadi lililopo Mashariki mwa Afrika.
Kundi hilo linalohusishwa na lile la Al-Qaeda, limekuwa likipigana na Serikali ya Somalia. Klabu ya Toulouse FC imetangaza uhamisho huo na kumshukuru Somalia kwa kile alichokifanya kwa kipindi chote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here