Usher atumia saa 3 kuchora ‘tattoo’

0
389

LOS ANGELES, MAREKANI 

MKALI wa muziki wa RnB nchini Marekani, Usher Rymond, ametumia saa tatu kuchora michoro nyuma ya shingo na kichwa chake.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 40, alikutana na mchoraji maarufu wa michoro jijinu Los Angeles, Dillon Forte na kuchora michoro hiyo ambayo inajulikana kwa jina la geometric patterns (Mifumo ya Kijiometri).

“Nimekuwa nikimsikiliza Usher akiimba tangu nikiwa na umri wa miaka 11, lakini leo ninajisikia kuwa na furaha kupata nafasi ya kufanya naye kazi, jambo la kujivunia kuniamini niweze kumchora mwilini mwake,” aliandika Forte kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Usher amekuwa kimya kwa muda mrefu, mara ya mwisho kuachia wimbo wake mpya ilikuwa Septemba 2016, ambapo aliachia wimbo wa Hard II Love, lakini amekuwa akionekana katika studio huko jijini California, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuachia wimbo mpya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here