26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Bieber aomba pambano na Tom Cruise

NEW YORK, MAREKANI 

STAA wa muziki wa pop, Justin Bieber, amewashtua mashabiki wake baada ya kuomba pambano la ngumi dhidi ya staa wa filamu, Tom Cruise.

Wawili hao wamekuwa wakijifunza ngumi mchanganyiko maarufu kwa jina la UFC, hivyo Bieber anaamini yupo tayari kwa ajili ya kushuka ulingoni ili kushindana na mpinzani wake huyo.

Bieber amekuwa rafiki wa karibu na bingwa wa ngumi duniani Floyd Mayweather, hata katika mazoezi yake, Mayweather amekuwa akimfundisha baadhi ya mbinu za kupambana na mpinzani wake.

“Nipo tayari kwa ajili ya kupambana na Tom Cruise. Tom kama hautokuwa tayari kukubali pambano hilo basi utakuwa unaniogopa, lakini nipo tayari kupambana na mtu yeyote atakaye kuwa tayari,” aliandika Bieber kwenye Instagram.

Bieber ana umri wa miaka 25, wakati huo mpinzani wake Tom ana umri wa miaka 56, lakini anaamini anaweza kumgalagaza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles