23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

Messi mwanamichezo anayelipwa zaidi duniani

NEW YORK, MAREKANI 

MSHAMBULIAJI wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, kwa mujibu wa Jarida la Forbes, ametajwa kuwa mwanamichezo anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani.

Messi mwenye umri wa miaka 31, ameripotiwa kuwa mwaka jana alilipwa jumla ya kiasi cha dola milioni 127, katika kipindi chote cha miezi 12 na kuwa mwanamichezo aliyeingiza fedha nyingi kuliko yeyote kati ya 100 waliotajwa.

Kwa upande mwingine mshambuliaji wa Juventus na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, akishika nafasi ya pili akilipwa dola milioni 109, huku mshambuliaji wa Paris St-Germain na timu ya taifa ya Brazil, Neymar akiingiza kiasi cha dola milioni 105.

Mwaka jana mwanamichezo aliyelipwa kuliko wote duniani alikuwa ni bingwa wa ngumi duniani Floyd Mayweather, lakini sasa ameshuka katika orodha hiyo na hayupo katika nafasi 10 za juu. 

Nafasi ya nne kwenye orodha hiyo inashikwa na Canelo Alvarez ambaye ni bingwa wa ngumi kutoka nchini Mexico mwenye umri wa miaka 28 anayecheza ngumi za uzani wa kati. Bondia huyo anachukua kiasi cha dola milioni 94.

Nyota wa mchezo wa tenisi Roder Federer ametajwa kushika nafasi ya tano akichukua kiasi cha dola milioni 93.4 kwa mwaka, wakati huo mchezaji wa mpira wa miguu wa Kimarekani, Russell Wilson ambaye ni mume wa msanii wa muziki Ciara, anashika nafasi ya sita akiingiza dola milioni 89.5, akifuatiwa na Aaron Rodgers mwenye dola milioni 89.3.

Nyota wa mchezo wa kikapu LeBron James, ametajwa kushika nafasi ya nane akiwa na kiasi cha dola milioni 89, wakati huo Stephen Curry akishika nafasi ya tisa akiwa na dola milioni 79.8 na nafasi ya 10 ikishikiliwa na nyota wa Golden State Warriors, Kevin Durant akiwa na dola milioni 65.4.

Mchezaji tenesi Serena Williams ni mwanamke pekee katika watu 100 wanaolipwa vizuri na kwa mujibu wa Forbes analipwa dola milioni 29.2 

Mshindi wa mara tano wa mashindano ya dunia ya magari ya Formula 1, Lewis Hamilton na mshindi wa zamani wa masumbwi uzani wa juu Anthony Joshua ndio wanamichezo wanaolipwa vizuri zaidi nchini Uingereza, wakichukua namba 13 na malipo yao ni dola milioni 55.

Jarida hilo la Marekani lilikokotoa malipo ya wanariadha kwa kujumlisha fedha za malipo ya tuzo, mishahara na nembo walizoidhinisha kati ya Juni 2018 na Juni 2019.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles