24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Usafiri majini marufuku siku ya uchaguzi

Usafiri majiniNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Usafiri  Baharini Zanzibar imefuta  safari zote za baharini siku ya uchaguzi wa marudio Zanzibar, Machi 20 mwaka huu  kutoa fursa kwa wananchi wenye sifa  kupiga kura visiwani humo.

Katika taarifa yake   jana, mamlaka hiyo ilisema siku hiyo ni marufuku kwa vyombo hivyo kusafirisha abiria kwa vile  hiyo ni fursa pekee kwa wananchi kushiriki uchaguzi huo.

Taarifa hiyo ilisema   uamuzi huo umefikiwa kutokana na wananchi wengi   kujiandikisha kupiga kura.

Machi 20 mwaka huu wananchi wa Zanzibar watachagua viongozi wa ngazi mbalimbali baada ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25  mwaka jana kufutwa kwa kile kinachodaiwa kuwa   kasoro wakati wa upigaji kura.

Matokeo hayo yalifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

Baadhi ya  vyama vya upinzani vimesusia uchaguzi huo wa marudio kikiwamo chama kikuu cha upinzani  cha CUF.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles