Ujerumani kuunga mkono mradi wa maji safi Tanga

0
596

Susan Uhinga, TangaSerikali ya Ujerumani imeonyesha kuridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maboresho ya huduma ya maji safi unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka ya jijini Tanga (Tanga Uwasa).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga leo Jumatatu Oktoba 8, kiongozi wa ujumbe kutoka nchini humo, Niels Breyer wameridhishwa na mradi huo na kwamba wataendelea kuunga mkono Jitihada za utekelezajinwa miradi ya maji safi.

“Tumekuja kutazama namna ambavyo wametekeleza mradi ambao tulisaidia na tumeridhishwa kwa asimilia kubwa jambo linalotusukuma kuendelea kushirikiana na mamalaka za maji katika kuhakikisha huduma za maji safi na maji taka zinaimarika,” amesema kiongozi huyo.

Kwa upande wake Ofisa Utafiti na Maendeleo wa Tanga Uwasa, Alawi Ahmad, amesema mradi huo umesaidia kuongeza kiasi cha maji kwa wateja wapato 1,000.

Katika katika mradi huo, Serikali ya Ujerumani Sh bilioni 1.23 ambayo ni sawa na riba ya mkopo wa Sh bilioni 3.6 ambao Uwasa walikopa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here