‘Mitandao inachangia ongezeko la wagonjwa akili’

0
1170

Susan Uhinga, TangaMatumizi mabaya ya mitandao yametajwa kuchangia ongezeko la wagonjwa wa akili na wengine kujiua.

Hayo yamebainishwa leo Jumatatu Oktoba 8, na Mratibu wa Afya ya akili Mkoni Tanga, Anita Temu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na masuala yanayochangia tatizo la afya ya akili.

Amesema kwa sasa Jamii imetekwa sana na mitandao jambo linachangia kuongezeka kwa kuwepo kwa ugonjwa huo.

“Vijana wengi wamekuwa wakitumia mitandao vibaya na muda mwingi wamekuwa wakiutumia huko jambo hili linasababisha shambulio la mtandao ambalo husababisha kutokea tatizo la afya ya akili.

“Tunawaasa wazazi kushirikiana na walimu katika malezi ya watoto lakini pia wazazi wanatakiwa kutenga muda kwa ajili ya kuzungumza na watoto wao kwani kwa kutokufanya hivyo kunajenga watoto wenye hasira hali inayopelekea kutokea kwa tatizo la afya ya akili kwa sababu sasa hivi mitandao ya kijamii imechukua nafasi kubwa jambo linalosababisha watoto kubaki wapweke wakishindwa kuwasilisha kero au mambo yanayowasibu kwa wazazi wao,” amebainisha Temu.

Pamoja na mambo mengine, Temu amesema kwa mwaka huu, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo, imepokea wagonjwa 75 ambao wanaugua tatizo la afya ya akili wengi wao  wakiwa vijana ambao tatizo hilo limetokana na utumiaji wa madawa ya kulevya na uvutaji wa bangi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here