Taswira halisi ya Taifa Stars kufuzu Afcon hii hapa

0
1873

NA MAREGES NYAMAKA-DAR ES SALAAM


ALFAJIRI ya leo timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilikuwa inatarajia kuanza safari ya kwenda Cape Verde kwa ajili ya mchezo wa kufuzu fainali za Afrika (Afcon)2019.

WazirI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, ameonekena kutokuwa mbali sana ya kikosi hicho, ambacho kipo chini ya kocha, Emanuel Amunike.

Hatua hiyo inatokana na Mwakyembe, kuwa msaada mkubwa wa upatikanaji wa usafiri wa ndege ya kisasa inayomilikiwa na Serikili Boeing 787-8 Dreamliner, jambo lililopokelewa kwa mikono miwili na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Wallace Karia.

Baada ya kuwasili viunga hivyo, kikosi hicho kinatarajia kushuka dimbani Septemba 12 kuumana na mwenyeji wake, kabla kurudiana siku nne baadaye katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo utakaochezwa kwenye ardhi ya Cape Verde (Estádio Nacional de Cabo Verde), utakuwa wa pili kwa kocha Mnigeria Amunike, tangu akabidhiwe majukumuu hayo na Karia Agosti 6 mwaka huu.

Amunike anayeonekana kuwa mwenye misimamo mikali, alianza kwa kuvuna pointi moja ugenini dhidi ya Uganda mchezo uliyomalizika kwa suluhu.Ni karata nyingine kwake dhidi ya Cape Verde.

Msimamo wa kundi hilo L lenye timu nne, unoanyesha wenyeji wetu Cape Verde ndiye anayeburuza mkia, baada kuambulia sare ya bao 1-1 mchezo uliyopita dhidi ya Lesotho, huku ule wa awali akitunguliwa bao 1-0 na Uganda.

Aina hiyo ya matokeo inatoa taswira kuwa kikosi hicho kinachonolewa na kocha mzawa wa taifa hilo, Lúcio Antunes tangu 2016, bado katika makatatasi mchezo ni 50/50.

Mchezo wa kwanza kilifungwa na timu bora zaidi, Uganda tena bao moja pekee ikiwa nyumbani, kabla ya kuvuna pointi moja ugenini wakisawazisha bao dakika 81 lililofungwa na mshambuliaji wao, Jorge Djaniny ‘Tavares Semedo’.

Semedo ambaye ngazi ya klabu anahudumu Al-Ahli ya Saudi Arabia, ndiye anayetajwa miongoni mwa mastraika wakali wanaotegemewa kikosini hapo kulingana na mahitaji ya kocha alivyowasoma wapinzani.

Hao hao Cape Verde katika viwango vya ubora duniani, orodha ya mwisho iliyotolewa na Shirikisho la Soka Kimataifa (FIFA) Septemba 20, wanashika nafasi ya 67,huku Tanzania tukiwa chini kabisa nafasi ya 140.

Mbali na kutuzidi kwa mbali sana kwa ubora huo wa viwango duniani,lakini kikosi hicho kina idadi kubwa ya wachezaji wanoacheza ligi kubwa nje ya mipaka yao ikiwamo wanandinga zaidi ya wanne wanaocheza Ligi Kuu nchini Ureno.

Miongoni mwa wachezaji hao wanaocheza Ulaya ni nahodha wao, Marco Paulo da Silva mwenye umri wa miaka 34, anaichezea Clube Desportivo Feirense inayoshikiri Ligi Kuu Ureno(Primeira Liga).

Ninachokitarajia kutoka kwa Taifa Stars yenye wachezaji tisa wanaocheza soka nje ya ardhi ya nyumbani,akiwamo nahodha Mbwana Samatta kutoka Genk,Ubeligiji ni uwajabikaji wa wao wenyewe unaombatana na nidhamu ya mchezo.

Masuala ya mfumo utakuotumiwa na Amunike sambamba na mbinu zake inabaki kuwa kazi yake kwa namna anavyolijua soka la Afrika, lakini pia akitambua wapinzani wake hao ambao kwa miaka ya karibuni wamekuwa shupavu sana.

Taswira ya kundi hilo ambalo ni timu mbili pekee zitakozopata nafasi ya kucheza michuano hiyo mwakani nchini Camerron zitakozokuwa zimekusanya alama nyingi zaidi, itakuwa wazi baada ya mechi mbili ndani ya wiki moja.

Licha ya utamaduni wa soka la Afrika, mwenyeji kuwa na asilimia kubwa ya kuvuna matokeo bora, bado Taifa Stars ina nafsi kubwa ya kufanya kitu ugenini kama si pointi zote tatu, angalau moja itakuwa inatuweka pia sehemu salama.

Mchezo wa marudiano wa Septemba 16, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hapo ndipo kwenye nafasi kubwa ya muelekeo wetu wa kufuzu fainali hizo kwa mara pili, baada ya miaka 30 iliyopita.

Matokeo ya mchezo huo yatakuwa yameacha mwanga mzuri au kwa Amunike katika mipango yake kuvuta pumzi kusubiri mechi mbili kuwakabili Uganda, Uwanja huo huo wa Taifa,lakini pia kuwafuata Lesotho hapo baadaye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here