Imechapishwa: Fri, Apr 21st, 2017

TYRESE AWAOMBA RADHI ALIOWAAHIDI NDOA

NEY YORK, MAREKANI


MSANII wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Tyrese Gibson, amewaomba radhi warembo wote aliowahi kutoka nao kimapenzi na kuwaahidi ndoa wakati akijua kwamba alikuwa akiwadanganya.

Msanii huyo kwa sasa amemuoa Samantha Lee, msichana ambaye hana umaarufu wowote na ndoa yao ilifungwa  kwa siri Februari mwaka huu na picha za harusi yao ziliwekwa hadharani baada ya siku kadhaa.

“Ndoa ni kitu cha siri, nimetoka na warembo wengi na nilikuwa nikiwaahidi kuwaoa lakini sikuweza kufanya hivyo na badala yake nimekuja kufunga ndoa na mwingine, hivyo nawaomba radhi kwa kutotimiza ndoto zao,” alieleza Tyrese.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

TYRESE AWAOMBA RADHI ALIOWAAHIDI NDOA