25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Tukibadili mfumo, wizi wa mitihani hautakuwapo

Na LEONARD MANG’OHA

HIVI juzi Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) lilitangaza matokeo ya darasa la saba, uliofanyika mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu, ambaoo Mkoa wa Dar es Salaam uliongoza kwa ufaulu.

Mwaka huu matokeo hayo yaligubukwa na kashfa mbaya ya wizi wa mitihani, tena wakihusishwa walimu, wasimamizi, walimu wakuu wa shule na maofisa elimu.

Mbali na Halmashauri wa Chemba ambayo matokeo ya shule zake zote yalifutwa, pia zilikuwamo baadhi ya shule binafsi.

Jambo la msingi tunalopaswa kujiuliza ni kwanini mitihani inaibwa tena ikihusisha walimu na maofisa wa serikali.

Kwa shule binafsi ni wazi kuwa hili linafanyika kwa sababu ya kibiashara ili kujiweka katika mazingira mazuri kuwavutia wazazi kuwaandikisha watoto wao katika shule hizo kwa imani kuwa ndizo shule bora hivyo kila mmoja kuvutiwa nazo.

Lakini jambo kubwa ninaloliona kuwa ni chanzo kikubwa cha janga hili ni kutokana na mfumo wetu wa elimu kuangalia viwango vya ufaulu wa mwanafunzi kwa alama alizopata katika mtihani wake badala ya stadi, maarifa na ujuzi anaoupata katika masomo yake.

Kutokana na hali hiyo, ndiyo maana mikoa ambayo imekuwa ikishindwa kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali imekuwa ikinyooshewa vidole na hata maofisa elimu wa maeneo husika na walimu wakuu kuchukuliwa hatua ikiwamo kushushwa madaraja.

Msukumo huu ndiyo unaosababisha walimu na maofisa elimu na wakati mwingine kamati nzima za halmashauri kushikiri katika udanganyifu huu ambao ni hatari kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa la leo.

Ili kuepuka kasoro hii, ni vema kuwa na mfumo wa elimu usiolenga ushindani wa ufaulu baina ya shule na shule au mkoa na mkoa badala yake tuwe na mfumo unaopima stadi, ujuzi na maarifa anayoyapata mwanafunzi kama vinamwezesha kukabiliana na changamoto za maisha kulingana na elimu aliyonayo.

Kama mfumo huu hautabadilishwa, ni wazi kwamba wizi huu wa mitihani utaendelea kushuhudiwa kwani upo ushahidi wa wazi siyo tu katika shule za kata bali hata zile za vipaji zimekuwa zikipokea wanafunzi ambao hata kusoma kitabu cha Kiingereza cha darasa la kwanza hawawezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles