30.8 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaoishi mabondeni watahadharishwa

                  Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

HALMASHAURI ya Manispaa ya Kigamboni imewataka wakazi wanaoisha katika maeneo hatarishi kuchukua tahadhari ikiwamo kuhama kabla mvua haijaanza   kuepuka kupatwa na maafa.

Tahadhari hiyo ilitolewa juzi na Meya wa Manispaa ya Kigamboni, Maabadi Hoja (CCM), wakati wa kikao cha cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani.

Alisema timu ya watendaji itafanya ukaguzi wa kuyaainisha maeneo hayo  kuangalia yana usalama gani.

“Wito wangu ni kwamba kila anayefahamu anaishi katika maeneo hatarishi anatakiwa aondoke kwa hiari kabla ya kupatwa na maafa,” alisema Hoja.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Ng’wilabuzu Ludigija, alisema zinafanyika jitihada za kukamilisha ujenzi wa shule mbili za sekondari ziweze kuwa na kidato cha sita.

Alisema shule moja ipo Kigamboni na nyingine katika eneo la Somangila ambayo tayari miundombinu yake yote imejengwa.

Alisema pia zimepokewa Sh milioni 500 kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ajili ya ujenzi wa hospitali eneo la Nafco na kwamba kupitia vyanzo vya ndani   ujenzi wa Kituo cha Afya Kimbiji unatarajiwa kukamilishwa.

Alisema pia yamepelekwa maombi maalumu i kupatiwa fedha za kumalizia ofisi za manispaa kwa kuwa walipopanga hapatoshi jambo linalosababisha usumbufu kwa watumishi katika kutekeleza majukumu yao.

“Tunafanya kazi katika mazingira magumu, watumishi wanafanya kazi hadi koridoni idara nyingine zimekosa ofisi.

“Tunaamini wakitupatia tutakamilisha angalau ghorofa moja tuhamie ifikakapo Februari mwakani,” alisema Ludigija.

Diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa, aliiomba manispaa hiyo kuendelea kuboresha miundombinu kwa kuyafanyia ukarabati maeneo yanayojaa maji.

Akijibu kero hiyo, Mhandisi wa Manispaa hiyo, Pius Mutechura, alisema maeneo hayo yatafanyiwa kazi   kuyaweka katika hali nzuri.

Alisema    mazungumzo na Bandari ya Dar es Salaam yanaendelea  waweze kupewa eneo la kituo cha magari kwa sababu  kilichopo kimekuwa kidogo kutokana na ongezeko la watu na magari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles