24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP: NITAJIONDOA MAZUNGUMZO NA KIM JONG-UN YASIPOLETA MATUNDA

FLORIDA, MAREKANI


RAIS Donald Trump amesema atajiondoa iwapo mazungumzo yake na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un hayatazaa matunda.

Katika mkutano wa pamoja na wanahabari mjini hapa juzi na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, viongozi hao walisema shinikizo dhidi ya Korea Kaskazini lazima liendelee ili isitishe utengezaji wa silaha za nyuklia.

Abe yupo hapa kwa mazungumzo na Rais Trump, ambaye awali alithibitisha Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi Marekani (CIA), Mike Pompeo, alifanya ziara ya siri Korea Kaskazini kukutana na Kim.

Trump alisema Pompeo aliweka mazingira ya uhusiano mzuri na Kim, ambaye alimwita ‘mtu mdogo’ na kwamba mkutano wao ulienda vizuri.

Mkutano huo uliadhimisha mawasiliano ya juu kati ya Marekani na Korea Kaskazini tangu mwaka 2000.

Kufikia Juni mwaka huu, mkutano kati ya Trump na Kim unatarajiwa kufanyika. Maelezo ikiwamo eneo litakaloandaa mkutano huo bado yanaendelea kufanyiwa kazi.

Trump alisema iwapo anadhani mkutano huo hautafanikiwa, basi hatoshiriki na kwamba iwapo mkutano huo utafanyika na hataona matunda yake basi atasimama na kuondoka.

“’Kampeni yetu ya shinikizo itaendelea hadi pale Korea Kaskazini itakapositisha utengezaji wa silaha za kinyuklia.

“Kama nilivyosema awali, nyota ya Korea Kaskazini itang’aa pale taifa hilo litakaposimamisha mpango wake wa nyuklia. Itakuwa sikukuu kwao na kwa ulimwengu,” alisema.

Abe kwa upande wake alisema amemtaka Trump kusaidia kuachiwa huru kwa raia wa Japan waliotekwa nyara na Korea Kaskazini miaka ya 1970 na 1980.

Suala hilo limeathiri kwa kiasi kikubwa uhusiano kati ya mataifa hayo mawili kwa miongo kadhaa.

Trump aliahidi kulifanyia kazi suala hilo na raia watatu wa Marekani wanaoshikiliwa Korea Kaskazini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles