TRA Tanga yapongezwa kudhibiti magendo

0
1029

Na Susan Uhinga, TangaMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Tanga, pamoja na taasisi zinazoshiriki kufanya  doria katika mwambao wa Bahari ya Hindi Ukanda wa Tanga imepongezwa kwa kufanikiwa kudhibiti biashara za magendo.

Hayo yameelezwa leo na Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde, wakati alipotembelea bandari ya Tanga na kukuta majahazi matano na mamlka hiyo yaliyokamatwa yakisafirisha bidhaa zinazoingia nchini kinyume cha sheria.

“Kupambana na biashara za magendo ni kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alipinga vikali biashara za magendo wakati wa utawala wake,” amesema Mavunde.

Pamoja na mambo mengine, Naibu Waziri huyo ameahidi kulifanyia kazi kwa kulifikisha mahali husika ombi la TRA Mkoani humo la kutaka kupatiwa boti kwa ajili ya kuimarisha doria za baharini ambapo amezikabidhi boti hizo kwa taasisi za serikali zinazojishughulisha na doria za baharini.

Awali akisoma taarifa fupi Meneja wa mamlaka hiyo mkoani Tanga, Masawa Masatu amesema mamlaka hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa boti ya doria kwa ajili ya kusaka wahalifu wa biashara za magendo wanaotumia bandari bubu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here