23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

SIRRO AONYA TRAFIKI  WANAOABUDU FAINI ZAIDI

NA  FRANCIS  GODWIN, IRINGA


 

MKUU wa Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro, amewataka askari wa usalama barabarani kutumia busara na si tu kuwapiga faini madereva bila kuwapa onyo na kuwa suala hilo si sahihi.

Akizungumza mjini Iringa jana, Sirro alisema pamoja na kuwa kuna dhana potofu  miongoni mwa jamii  kuwa askari  hao wamepangiwa kiasi  cha fedha za kukusanya kwa siku, jambo  hilo si  kweli.

“Hakuna  askari wa  usalama  barabarani anayepangiwa makusanyo  ya  faini, IGP ni   mmoja nchi  hii,  mimi  ndio IGP nasema hakuna IGP anayepangia askari wa  usalama barabarani pesa, labda wana IGP wao  nyumbani  kwao,” alisema.

Alisema  kazi ya  askari  hao ni kusimamia sheria  za  usalama barabarani na  si  kila kosa  ni la kumpiga mtu  faini, na kwamba ni lazima busara  itumike  ikiwa ni pamoja na kumpa onyo mhusuka  pamoja na elimu kabla ya  kukimbilia  kumpiga  faini .

“ Jambo la  kwanza la  kuzuia  uhalifu ni  elimu kwanza, siku ya  pili onyo na siku ya  tatu ni faini,  sio unaanza kwa faini  pasipo kumpa  elimu wala  onyo.

Wakati  mwingine hawa  polisi  si malaika  yawezekana  wametoka nyumbani wakiwa ovyo,  hivyo  wanahamishia hasira  zao kwenye  faini,  ila naomba muwaelewe  hawa ni  watoto  wetu tuwasamehe bure ila ninachosisitiza elimu kwanza,  ukiona dereva kaongeza  spidi kwanza  mpe  elimu,” alisema.

Katika hatua nyingine, alisema haoni changamoto  kufanya kazi na  wanasiasa  kwani  wanasiasa  ni  sehemu ya jamii na  wanafanya  siasa  kwa mujibu wa  sheria  na kwamba hakuna aliye juu ya sheria.

“Hakuna mwanasiasa  aliye juu ya  sheria,  akikiuka  sheria atawajibika kwa mujibu wa  sheria  na  atashughulikiwa kama  mtu mwingine yeyote, hivyo hakuna  mwanasiasa atakayenisumbua  mwanasiasa  atakayetoa  lugha ya  matusi atakamatwa  tu  kazi yangu ni rahisi  sana kwa  kuwa nasimamia  sheria,” alisema.

Kuhusu uboreshaji wa nyumba  za askari  polisi  nchini  alisema  kuwa kuna  programu maalum ya  kuboresha   makazi ya  askari  polisi kupitia  fedha wanazopata  .

“ Nimefurahi sana kuwafahamu  nimekuwa  nikisoma tu  nondo  zenu  ila   leo  nimewafahamu  ahsanteni  sana  ila naombeni  jaribuni  kuandika  kile ambacho  nimesema  kuna mmoja jana  Mbeya ameandika  IGP anasema wana Siasa  wasiongee hii si  kweli  mimi siwezi  kuwazuia  wanasiasa kuongea  wazungumze tu  ila  wasivunje sheria,” alisema.

Kuhusu kauli  mbali mbali ambazo  amekuwa  akiziandika kwenye  mitandao ya   kijamii Mange  Kimambe alisema kuwa kauli  zake  hizo zimekuwa  zikivunja  sheria  ndani ya  nchi  ila mpango wa Jeshi la Polisi kuhusu mtu huyo hawezi  kusema kwa  sasa .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles