30.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 6, 2024

Contact us: [email protected]

TIC YAMSHANGAA DANGOTE KULALAMIKA

Na JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM


KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema kilitegemea mfanyabiashara maarufu barani Afrika, Aliko Dangote, atakuwa mtu wa mwisho kulalamikia sera za uwekezaji kutokana na upendeleo aliopewa hapa nchini.

Mbali na hilo, TIC imesema taarifa zilizotolewa na Mwandishi wa Financial Time (FT), John Aglionby, kuhusu Tanzania kuwa na mazingira hatarishi kwa wawekezaji si sahii na inalenga kupotosha ukweli juu ya hali halisi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geoffrey Mwambe alisema maelezo hayo ambayo ilielezwa kuwa ni ya tajiri namba moja Afrika, Aliko Dangote, yamelenga kupotosha sera za uwekezaji na kuwaogopesha wawekezaji ambao wameendelea kuiamini Tanzania na kuwekeza mitaji mikubwa.

“Tunatarajia Dangote awe mtu wa mwisho kulaumu, kwani Serikali imejitahidi kumwekea mazingira bora ya uwekezaji hasa pale Rais alivyoshugulikia suala lake la kupata gesi kwenye kiwanda chake, pia kuruhusiwa kuchimba mwenyewe makaa ya mawe kama hatua ya kuondoa mzunguko mkubwa uliokuwapo.

“Isitoshe Dangote mwenyewe wakati akihojiwa kwenye kituo kimoja nchini Uingereza alisema yeye hakumtuhumu  Rais Dk. John Magufuli, bali alizungumzia hali ya uwekezaji katika nchi za Afrika ziweze kuboresha mazingira na sera za uwekezaji kila wakati hivyo maelezo yaliyotolewa na mwandishi huyo si ya Dangote,” alisema.

Mwambe alisema TIC haiamini kama Dangote anaweza kuwa msemaji wa sekta ya madini hasa ukilinganisha uwekezaji wake ni kwenye sekta ya viwanda hususani saruji na serikali imekuwa mstari wa mbele kusikiliza na kufanyia kazi maoni ya mfanyabiashara huyo.

Alisema kwa sasa hivi Tanzania ipo katika vita ya kiuchumi hivyo mabadiliko ambayo yanaendelea kufanywa na Serikali wapo baadhi ya watu huko duniani hawayataki hususan kwenye sekta ya madini.

Aidha alisema makala hiyo inajionyesha wazi kuwa mwandishi hafahamu vizuri sheria ya uwekezaji ya mwaka 1997 ambayo inatambua umiliki binafsi wa mali na kuzuia uwezekano wa kutaifisha mali hizo bila sababu za msingi wa kisheria.

Alisema katika kuboresha mazingira ya uwekezaji wanaendelea kufanya marekebisho ya sera pamoja na sheria ili ziweze kuwa na manufaa kwa wote na kwamba Kiuto kimeendelea kupokea wawekezaji kutoka nchini mbalimbali na Tanzania imekaribishwa baadhi ya nchi kwenda kukutana na wawekezaji.

“Tanzania ni mahali salama kwa uwekezaji ndio maana kituo cha uwekezaji kimeendelea kuwa kikitingwa (buzy) kupokea wawekezaji mbalimbali hivyo nashang’aa hizi taarifa zinatoka wapi.

“Kwenye ripoti ya (IMC) inaonyesha Tanzania katika vipimo vya kimataifa kuhusu uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji imepanda nafasi saba hadi kufikia 144,” alisema Mwambe.

Alisema changamoto ambazo zipo kama vile miundombinu na umeme, serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha inaboresha ikiwamo ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge), kuboresha mfumo wa usajili wa makampuni BRELA, mradi wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge, ujenzi na ukarabati wa barabara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles