24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

RUANGWA DISTRIBUTER YATOA MSAADA WA MAMILIONI KWA WAJASIRIAMALI

Hadija Omary, Lindi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewakabidhi mkopo wa fedha taslimu Sh milioni tisa kwa akina mama lishe na baba lishe 42 wa Wilaya ya Ruangwa, mkoani hapa ambazo zimefadhiliwa na Kampuni ya Ruangwa Distributer Limited inayojishughulisha na uuzaji wa soda ya Coca Cola.

Wajasiriamali hao walipatiwa mkopo ni kutoka katika kata za  Narung’ombe, Matambalale, Namichiga, Mbekenyela, Nambilanje, Mandawa na Chimbila ambapo marejesho ya mikopo hiyo yatatakiwa kurejeshwa kwa kipindi cha miezi mine.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi ya kukabidhi mikopo kwa wajasiriamali hao iliyofanyika katika Kata ya Dodoma Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Majaliwa alimshukuru Mkurugenzi wa kampuni hiyo kwa uamuzi wake wa kutenga fedha kutoka katika vyanzo vyake kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa wajasiriamali.

“Natoa wito kwa wafanyabiashara wengine wakubwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wafanyabiashara kama hawa lakini pia niwasisitize walengwa wa mikopo hiyo kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa sanjari na kurejesha mikopo kwa wakati ili kuwapa fursa wajasiriamali wengine kupata mikopo hiyo,” amesema Majaliwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Ruangwa Distributer, Abdalah Mang’onyola amesema kampuni yake imefanya hayo kwa kutambua jitihada zinazofanywa na serikali za kuwainua wananchi kiuchumi huku ikiunga mkono kauli mbiu ya serikali ya ‘Hapa Kazi Tu’.

“Kwa kipindi cha mwaka 2018/19 kampuni yetu imetenga Sh milioni 10 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wanaojishughulisha na biashara ya chakula ambayo Waziri Mkuu leo utakabidhi Sh milioni tisa na milioni moja iliyosalia haitatolewa leo kwa kuwa uhakiki wa kuwapata wanaostahili na mkopo huo haukukamilika,” amesema Mang’onyola.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles