26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

DK. KALEMANI AMUOMBA MUNGU AILAZE SERIKALI MAHALI PEMA PEPONI

Paul Maregesi, Dodoma

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amewavunja mbavu wabunge baada ya kuwaambia anamuomba Mwenyezi Mungu aiweke serikali mahala pema peponi.

Dk. Kalemani ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma leo Mei 25, alipokuwa akihitimisha mjadala wa Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/19 aliyowasilisha jana.

Kabla ya kusema hayo Dk. Kalemani alikuwa akieleza jinsi serikali ilivyotekeleza miradi mbalimbali na kuwapelekea wananchi umeme katika maeneo mbalimbali nchini ambapo alijikuta akisema: “namuomba Mwenyezi Mungu aiweke serikali mahali pema peponi,”.

Hatua hiyo iliwafanya wabunge kuangua vicheko huku Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu akilazimika kuwatuliza wabunge na kuwataka waendelee kumsikiliza waziri badala ya kucheka.

Hata hivyo, baada ya dakika chache Dk. Kalemani alisema anamuomba Mwenyezi Mungu aibariki serikali na kuwafanya wabunge kucheka tena kwa sauti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles