24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS PUTIN AMTUMIA SALAMU ZA PONGEZI KIM JONG-UN

MOSCOW, Urusi


RAIS wa Urusi, Vladimir Putin, amemtumia ujumbe wa salamu za pongezi mwenzake wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, kwa taifa hilo kutimiza miaka 70 ya kuanzishwa kwake.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA), Rais Putin alituma salamu hizo za pongezi jana kwa njia ya telegram akieleza kuwa ana uhakika mataifa haya mawili yataendelea kushirikiana katika nyanja mbalimbali.

Shirika hilo lilieleza kuwa katika salamu hizo, Rais Putin alielezea pia kwamba ana uhakika Serikali za Moscow na Pyongyang zitafanya mazungumzo ya kimataifa yatakayosaidia kujenga  ushirikiano  zaidi katika nyanja hizo mbalimbali.

“Nakupongeza kwa kuadhimisha  kumbukumbu ya miaka 70 ya  kuanzishwa Jamhuri ya Demokrasi ya Watu wa Korea Kaskazini, DPRK. Nasema tuna uhusiano mkubwa na wa kuridhisha baina ya Serikali ya Urusi na DPRK,” Shirika hilo la KCNA liliukariri ujumbe huo.

“Uhusiano huu unatimiza kikamilifu masilahi ya watu wa nchi zetu na unasaidia kuimarisha hali ya utulivu na usalama kwenye Peninsula ya Korea na  Kaskazini na bara kwa ujumla,” uliongeza ujumbe huo.

Shamrashamra za maadhimisho hayo ya miaka 70 zilifanyika jana katika mji mkuu wa nchi hiyo, Pyongyang na kuhudhuriwa na viongozi kutoka mataifa mbalimbali ambapo Urusi iliwakilishwa na Spika wa Bunge, Valentina Matviyenko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles