24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

KOREA KASKAZINI YAANDAA GWARIDE BILA MAKOMBORA

PYONGYANG, Korea Kaskazini 


SERIKALI ya hapa jana haikuonesha makombora ya masafa marefu kwenye gwaride la jeshi ambalo lilifanyika mjini hapa ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 70 ya kuanzishwa taifa hili.

Mbali na kutoonesha silaha hizo za masafa marefu, pia haijulikani kama kiongozi wa nchi hii, Kim Jong-un, alitoa hotuba kwenye warsha hiyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, gwaride hilo lilikuwa linafuatiliwa kwa karibu ili kufahamu iwapo Serikali ya Pyongyang imejitolea kuharibu zana zake za nyuklia.

Kabla ya gwaride hilo, baadhi ya wachambuzi walikuwa wametabiri kuwa Rais Kim angepunguza maonyesho ya silaha kufuatia mkutano na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Maonyesho makubwa ya makombora ya masafa marefu ambayo yanaweza kufika nchini Marekani na yenye  uwezo wa kubeba mabomu ya nyuklia yanaonekana kama uchokozi.

Juni mwaka huu marais Kim na Trump, walisaini makubaliano kufanya kazi katika kumaliza silaha za nyuklia kutoka rasi ya Korea lakini hakukuwa na mpangilio wa kufanya hivyo.

Mazungumzo ya kiwango cha juu yameendelea lakini ziara ya hivi majuzi ambayo ingefanywa na Waziri wa Mashauri ya Nchi za Kigeni wa Marekani, Mike Pompeo, ilifutwa dakika za mwisho huku pande zote zikilaumiwa kwa kukwama mazungumzo hayo.

Korea Kaskazini pia ilitarajiwa kufanya mazoezi makubwa ya kijeshi kwa miaka mitano. Na uchunguzi wa kutumia satelaiti kutoka wiki mbili zilizopita unaonyesha kuwa maonyesho hayo ya mwaka huu yataendelea hadi mwezi wote wa Septemba na yatakuwa makubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles