RAIS AL BASHIR KUWAUNGANISHA KIIR, MACHAR

0
347

Rais wa Sudan, Omar Al- Bashir anadaiwa kuwa tayari kuandaa mazungumzo ya amani kati ya mahasimu wawili wakuu wa Sudan Kusini, Rais Salva kiir na Riek Machar.

Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Sudan ilitangaza kwamba ilitangaza pendekezo la Rais Bashir liliwasilishwa kwa Rais Kiir na ujumbe wa Sudan uliotembelea Juba Jumanne wiki hii ikiwa ni siku chache baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha azimio linalozipatia pande zinazogombana Sudan Kusini mwezi mmoja kufikia makubaliano ya amani au kukabiliwa na vikwazo vikali zaidi.

​Ujumbe wa Sudan uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Sudan, Al- Dierdiry Al-dhikheri.

Rais Salva Kiir anaripotiwa kuthibitisha serikali yake iko tayari kushiriki kwenye mazungumzo hayo ingawa siku bado haijatajwa.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here